Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 09:18

Polisi wawasaka wahusika na kusema shambulizi la London ni la kigaidi


Polisi wakiwa katika eneo la mlipuko huko London wakiwa wanafanya uchunguzi.
Polisi wakiwa katika eneo la mlipuko huko London wakiwa wanafanya uchunguzi.

Mlipuko wa ghafla uliotokea London kwenye kituo cha treni cha Parsons Green leo ijumaa majira ya asubuhi limejeruhi takriban watu 22 ambao polisi wameeleza kuwa ni shambulizi la kigaidi.

Mark Rowley, kamishna naibu msaidizi wa kituo cha polisi cha Metropolitan London amewaambia waandishi wa habari kuwa inaelekea mlipuko huu ulikuwa umekusudiwa.

Baada ya uchunguzi wa awali, Rowley aliwaambia waandishi kuwa: “ Hivi sasa tathmini yetu inaonyesha kuwa bomu hili lilikuwa limetengenezwa kienyeji.

Wanaoshughulika na huduma za dharura katika tukio hilo wamesema hakuna majeraha yaliyo onyesha tishio kwa maisha ya watu waliokumbwa na shambulizi hilo.

Idara inayosimamia magari ya kuhudumia wagonjwa London inasema wafanyakazi kadhaa wamepelekwa kwenye eneo kuwahudumia wale waliokuwa wamejeruhiwa.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema kwamba mlipuko huo ulisababisha mkanyagano na kupelekea mtaharuki mkubwa kwa watu waliokuwa katika kituo cha treni cha chini ya ardhi ambacho ni maarufu kwa jina la "theTube" nchini Uingereza.

Polisi wa mji huo wanasema idadi kadhaa ya maafisa wataalamu wa kupambana na kuchunguza tukio la ugaidi wako tayari kwenye tukio hilo huko West London.

Picha zilizopostiwa katika mitandao ya jamii zinaonyesha ndoo ikiwaka moto ambayo ilikuwa imewekwa ndani ya mfuko wa plastiki karibu na mlango wa treni.

XS
SM
MD
LG