Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 03, 2024 Local time: 21:31

Vanessa akabiliwa na shutma za dawa za kulevya


Paul Makonda
Paul Makonda

Polisi mkoa wa Dar es Salaam wanamshikilia msanii maarufu na mtunzi wa nyimbo, Vanessa Mdee, maarufu kwa jina la Vee Money, kwa madai ya kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya.

Wakili wake, Aman Tenga amethibitisha Jumatano kwamba mteja wake alijisalimisha mwenyewe kituo cha Polisi cha kati, baada ya kuwa ameorodheshwa kati ya wanaoshukiwa kuwa wanatumia madawa na kujishughulisha na biashara hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda mwezi uliopita alitangaza majina waliotakiwa kuripoti polisi likiwemo jina la msanii Mdee.

Wakili Tenga amefafanua kwamba mteja wake alikuwa Afrika Kusini kikazi wakati alipotajwa na mkuu wa mkoa. Pia amethibitisha kuwa polisi walisachi nyumbani kwa Mdee huko eneo la kunduchi.

Baada ya hapo Mdee alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa serikali kwa uchunguzi zaidi na baadae kuwekwa rumande.

Msanii huyo ambaye alizaliwa mwaka 1988 Arusha, alipata umaarufu kama matangazaji wa radio na TV, akiendesha vipindi vya Epic Bongo Star Search na Dume Challenge kwa kituo cha televisheni cha ITV Tanzania.

Pia kabla ya hapo aliwahi kusaini mkataba wa muziki na kikundi cha B’hitts Music Group mwishoni mwa mwaka 2012.

XS
SM
MD
LG