Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 01:40

Polisi Tanzania wapiga marufuku mikutano ya kisiasa


Askari polisi wa Tanzania alinda doria wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015. Polisi walipiga marufuku mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kote nchini kuanzia siku ya Jumatano kwa madai ya kwamba mikutano hiyo inatumika kuchochea uvunjifu wa amani.
Askari polisi wa Tanzania alinda doria wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015. Polisi walipiga marufuku mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kote nchini kuanzia siku ya Jumatano kwa madai ya kwamba mikutano hiyo inatumika kuchochea uvunjifu wa amani.

Na Dinah Chahali,

Polisi wa Tanzania siku ya Jumatano walitangaza pigwa marufuku kwa mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kote nchini kwa madai ya kwamba mikutano hiyo inatumika kuchochea uvunjifu wa amani.

Hatua hiyo imefuatia vikao vya ndani vinavyofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwenye maeneo mbalimbali nchini katika maandalizi ya opreseheni waliyoiita ya kupinga udikteta Tanzania , UKUTA.

CHADEMA wamepanga kufanya maandamano na mikutano ya hadhara nchini nzima septemba mosi mwaka huu

Wakati huo huo, polisi nchini tanzania wamezungumzia juu ya mauaji ya askari wanne wa jeshi hilo yaliyotokea jana kata ya Mbande Temeke jijini DSM huku ikikataa kuhusisha tukio hilo na ugaidi au ujambazi bali shambulio dhidi ya askari wake

Askari waliouawa katika tukio hilo ni Koplo Yahaya ,Koplo Hatibu Koplo Tito na Koplo Gastone huku raia Raia waliojeruhiwa wakifahamika kwa majina ya Ally Chiponda na Azizi Yahaya wote Wakazi wa Mbande

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam kuhusiana na tukio hilo ambapo licha ya mauaji hayo silaha mbili aina ya SMG na risasi 60 ziliporwa, Kamishna Operesheni na Mafunzo kutoka Makao Makuu ya Polisi Nsato Marijani Mssanzya amesema upelelezi wa kina juu ya tukio hilo unaendelea

XS
SM
MD
LG