Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 09, 2022 Local time: 09:22

Polisi New York wamhoji dereva wa shambulizi la kigaidi


Kamishna wa Polisi New York Police James P. O'Neill akizungumza na waandishi Jumatano, Novemba 1, 2017,

Vyombo vya usalama katika jiji la New York Jumatano wameendelea kumhoji dereva wa gari la aina ya pickup ambaye aliwagonga watu katika sehemu iliyokuwa na harakati nyingi za wanaoendesha baiskeli Jumanne.

Vyombo hivyo vinajaribu kutafuta kitu kilichopelekea mtu huyu kufanya shambulizi hili la kinyama la kigaidi katika jiji ambalo tukio kama hilo la kigaidi liliwahi kutokea wakati wa Septemba 11, 2001.

Wakati huohuo maafisa wa jiji hilo na wakazi wake wameahidi kuwa shambulizi hilo haliwezi kuwatishia wakazi wa New York.

Kitengo cha uchunguzi cha polisi walikuwa bado wako katika eneo la tukio Jumatano, wakichunguza gari iliyofanya shambulizi hilo ikiwa inatembea kwa mwendo kasi katika njia iliyotengwa kwa ajili ya wapanda baiskeli.

Tukio hilo lilitokea upande wa magharibi wa New York, na kuwagonga waliopanda baiskeli, watembea kwa miguu na hatimaye kuligonga basi la shule. Katika matukio hayo, watu wanane waliuwawa na wengine 20 kujeruhi baadhi yao vibaya sana.


Facebook Forum

XS
SM
MD
LG