Tukio hilo linaelezwa kuwa ni la uovu mkubwa lililo sababisha vifo katika jiji hilo tangia kutokea kwa shambulizi la Septemba 11 mwaka 2001.
Takriban watu wanane wamefariki dunia na wengine 11 kujeruhiwa katika kile meya wa jiji hilo Bill de Blasio alichokiita kitendo cha kigaidi cha mtu mwoga kushambulia raia wasio na hatia.
Maafisa wa polisi walioongea kwa masharti ya kutatambulishwa, wameviambia vyombo vya habari kwamba mshukiwa ni muhamiaji kutoka nchi ya Uzbekistan, Sayfullo Saipov, mwenye umri wa miaka 29 ambaye aliingia Marekani 2010 na alikuwa mkazi wa jimbo la Florida.
Kwa upande wake Gavana wa New York Andrew Cuomo ameeleza shambulio hilo limetekelezwa na mtu mpweke, akisema hakuna ushahidi unaoonyesha lilikua sehemu ya mpango mkubwa zaidi.
Tukio hilo lilitokea katika njia ya wapita baiskeli na watu wanaotembea kwa miguu karibu na eneo la makumbusho ya World Trade Center kusini mwa kisiwa cha Manhattan, kulikotokea mashambulio ya kigaidi ya Septemba 11, 2001.
Kamishna wa polisi wa New York James O'Neill amasema ilikua karibu saa tisa za mjioni wakati dereva akiwa na lori dogo alipopita katika njia hiyo ya kupita baiskeli, akiwagonga watu wanaopita. .