Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 08:02

Picha rasmi za Obama, Michelle zazinduliwa


Rais mstaafu Barack Obama na mchoraji Kehinde Wiley, kushoto, wakizindua picha rasmi ya Obama.
Rais mstaafu Barack Obama na mchoraji Kehinde Wiley, kushoto, wakizindua picha rasmi ya Obama.

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle Obama walionekana pamoja katika fursa adimu walipohudhuria mjini Washington, Jumatatu, uzinduzi wa picha zao rasmi katika maonyesho ya picha katika Jumba la kumbukumbu za picha la kitaifa la Smithsonian.

Sanaa hizo zilizinduliwa katika chumba maalum cha maonyesho ya picha, ambacho kimehifadhi picha zote za marais.

Picha ya mkewe Obama ilizinduliwa kwanza. Alimchagua mchoraji wa Baltimore Amy Sherald kuchora picha hiyo. Sherald ni mshindi wa kwanza wa maonyesho ya mwaka 2016 yanayojulikana kama Outwin Boodh

Akionyesha furaha yake kwa kazi nzuri ya uchoraji wa picha yake, mkewe Obama amesema amekosa neno la kuelezea furaha yake.

Picha ya Rais mstaafu Obama ilichorwa na Kehinde Wiley, mwana Sanaa mashuhuri sana kwa picha zake zenye uhai, na picha kubwa zilizochorwa za Wamarekani weusi.

Obama amesema ameguswa sana na anashukuru kwa kupewa heshima hiyo:

“Nataka kumshukuru kila mtu aliyeko hapa, Michelle na Mimi tunawashukuru marafiki na familia, na wafanyakazi wenzetu wa zamani na hivi sasa, ambao watoa muda wao kuhudhuria hafla hii na kutupongeza kwa njia hii na kutengeneza Sanaa isiyo ya kawaida ambayo tunaishuhudia leo. Hii inamaana kubwa sana kwetu sisi na bila shaka nyinyi mnalifahamu hili. Tunaupweke kwa kutokuwa na nyinyi rafiki zetu, na…”

Imeelezwa kuwa Obama na mkewe walipitia picha zaidi ya dazeni mbili za wasanii kabla ya kuamua kuzikubali za Wiley na Sherald.

Picha ya Obama itatundikwa katika ukumbi wenye picha za marais, na ile ya mke wa Obama itawekwa katika kumbi nyingine. Picha zote mbili zitakuwa tayari kuangaliwa na umma kesho Jumanne.

XS
SM
MD
LG