Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 11:07

Marekani yatoa sharti la kuzungumza na Korea Kaskazini


Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson (kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje Sameh Shoukry

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Jumatatu kuwa mazungumzo yoyote ya Korea Kaskazini juu programu za makombora yake ya balistiki na nyuklia yatafanyika tu iwapo nchi hiyo itaonyesha iko tayari kufanya mazungumzo yenye tija.

Tillerson aliongea katika mkutano wa waandishi wa habari akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry baada ya wanadiplomasia hao wawili kuzungumzia masuala ya usalama wa eneo inayohusisha nchi ya Libya na Syria, pamoja na mchakato wa amani wa Israeli na Palestina.

Waadishi walitumia fursa hiyo kumuuliza waziri wa mambo ya nje kama anaona kunamustakbali wa kuwepo mazungumzo kati ya Marekani na Korea Kaskazini.

“Ni mapema sana kutoa maoni. Kama tulivyo kuwa tumesema kwa muda sasa, ni juu ya Korea Kaskazini kufanya maamuzi wakati watapokuwa tayari kuzungumza nasi kwa nia ya kweli, na njia yenye tija. Wanajua nini kinatakiwa kuwepo katika meza ya mazungumzo. Tumekuwa tukieleza kwa muda sasa kwamba nafikiri ni muhimu tuwe na majadiliano, na tutatakiwa tuwe na majadiliano fulani ambayo yatatangulia mazungumzo hayo.”

Tillerson amewataka wananchi wa Misri kuwa na imani na utayari ulionyeshwa na Marekani kuendelea kuisaidia Misri katika kupambana na ugaidi.

Tillerson anatarajiwa kukutana na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sissi mwanzoni mwa ziara yakeya Mashariki ya Kati.

Huko Kuwait, mwanadiplomasia wa juu wa Marekani ataongoza ujumbe katika mkutano wa mawaziri unaowaleta pamoja wanachama 74 wamuungano wa kuwatokomeza kikundi cha kigaidi cha ISIS.

Pia atahudhuria Mkutano wa Kuijenga tena Iraq, ambao unafanyika kwa mara ya kwanza tangia kikundi cha Islamic State kilipo ondolewa eneo la Raqqa, Syria na Iraq ikatangaza kuwa imeyakomboa baadhi ya maeneo yake.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG