Watu wa kabila la Rohingya wamekimbia kutoka Burma kwenda Bangladesh baada ya kukabiliwa na mashambulizi yanayotokana na uvunjifu wa amani.
Kauli ya Pence ni ya kipekee juu ya mgogoro huu na haijawahi kutolewa kwa kemeo kama hilo na kiongozi yoyote wa Marekani tangu mgogoro wa Waislam wa kabila la Rohingya nchini Myanmar utokee.
Akizungumza katika mkutano wa walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa Jumatano, Pence amesema ulimwengu unashuhudia “maafa makubwa yakijitokeza” katika taifa hilo la Kusini Mashariki mwa Asia ambalo pia linajulikana kama Burma.
Hivi Karibuni vikosi vya usalama vya Burma vilijibu mashambulizi ya waasi ambayo yalifanyika katika vituo vya serikali kwa ukatili usiokifani, wakichoma vijiji, na kuwafukuza watu wa Rohingya kutoka katika makazi yao,” amesema Pence katika mkutano wa Baraza la Usalama wa ngazi ya juu.
“Picha za uvunjifu wa amani na wahanga wake zimewashitua watu wa Marekani, na watu wastaarabu wa dunia nzima," pence alisema katika mkutano huo.
Facebook Forum