Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 16:44

Thailand : Papa Francis awataka maaskofu kuwa karibu na mapadri


Askofu Joseph Prathan Sridarunsil akiwa na Papa Francis alipozuru Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Peter huko Wilaya ya Sam Phran ya Jimbo la Nakhon Pathom, Thailand, Novemba 22, 2019. REUTERS/Remo Casilli

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewataka maaskofu nchini Thailand kuacha milango yao wazi kwa mapadri na kutangaza Injili kama walivyofanya wahuburi waliokuwa kabla yao.

“Kueni karibu na mapadri wenu, na wasikilizeni na shirikianeni nao katika kila hali, hasa pale mnapowaona wamekatishwa tamaa au hawanashauku tena na kazi yao, hali ambayo ni jaribio ovu la shetani kuliko yote.

Fanyeni hivyo siyo kama mnaotoa hukumu lakini kama mababa, na sio kama mameneja mnaowatuma, lakini kama kaka zao wakubwa wa kweli.”

Francis alitoa hotuba katika Mkutano wa Maaskofu wa Asia katika eneo takatifu la Nicholas Bunkerd Kithamrung huko Sam Phran, kilomita 56 magharibi ya mji wa Bangkok.

Kundi kubwa wakiwemo waumini kutoka Vietnam, Cambodia na China walimkaribisha Papa mapema alipowasili kukutana na mapadri na wanafunzi wanaosomea upadri katika Parokia ya Mtakatifu Peter huko Jimbo la Nakhon Pathom.

Francis alihitimisha siku ya sherehe hizo za ziara yake kwa Misa iliyokuwa imewakusudia vijana katika Kanisa la Bangkok.

Francis ni papa wa pili kutembelea Thailand. Papa John Paul II, ambaye sasa ni Mtakatifu John Paul II, alikuwa wakwanza kuzuru nchi hiyo mwaka 1984.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG