Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 14:55

Papa Francis atetea uamuzi wake wa kukataa kukubali kujiuzulu kwa Kardinali wa Ufaransa


Papa Francis akifanya ibada ya misa huko Prince Moulay Abdellah sports complex mjini Rabat, Morocco, March 31, 2019.
Papa Francis akifanya ibada ya misa huko Prince Moulay Abdellah sports complex mjini Rabat, Morocco, March 31, 2019.

Papa Francis Jumapili alitetea uamuzi wake wa kukataa kukubali kujiuzulu mapema mwezi huu kwa Kardinali wa Ufaransa Philippe Barbarin,ambaye anashitakiwa kwa kushindwa kutoa taarifa juu ya manyanyaso ya kingono kwa Polisi.

Papa Francis, ambaye alizungumza na waandishi wa habari akitoka katika ziara yake nchini Morocco, amesema uamuzi wa mwisho hauwezi kufanyika mpaka pale rufaa ya kardinali huyo itakaposikilizwa.

“Siwezi kukubali kwasababu katika maneno ya kisheria. duniani katika mfumo wa sheria kuna kutambuliwa kuwa huna hatia alimradi shauri lako bado liko mahakamani na umekata rufaa Papa alisema.

Barbarin aliomba kujiuzulu nafasi yake Machi 18. Na akasema kwa wakati huo Papa alisema anatambua kutokuwa hatia mpaka pale kesi itakapokamilika na kukataa ombi hilo.

Imetayarishwa na Sunday Shomari.

XS
SM
MD
LG