Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 01:17

Papa Francis aungana na vijana kupitia mtandao wa jamii


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akisalimia kundi kubwa la watu nje Ofisi yake Vatican, Jumapili Januari 20, 2019.
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akisalimia kundi kubwa la watu nje Ofisi yake Vatican, Jumapili Januari 20, 2019.

Wakati Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis akijitayarisha kukutana na maelfu ya vijana kutoka kote ulimwenguni kwa ajili ya “siku ya vijana” wiki hii, amefanya jitihada ya kuungana nao kwenye jukwaa la mtandao wa kijamii - intaneti ambalo watamuelewa kwa urahisi.

Katika sala ya kila wiki ya Angeluis, huko Vatican, jana Jumapili, kiongozi huyo wa kiroho Francis alizindua jukwaa la app yake ya “Click to Pray” ambayo ni rasmi hivi sasa kwa ajili ya mtandao wa sala zinazo endeshwa na Vatican duniani .

Kwa msaada wa msaidizi wake aliyekamata kifaa cha kielekroniki aina ya tablet, baba mtakatifu aligusa kioo cha tablet akisema kwa maneno yake, "hapa ndio mahala nitaweka maombi kwa ajili ya sala kwa shughuli za kanisa."

Baba mtakatifu aliwaambia waumini huko katika uwanjwa wa St. Peters square kwamba mitandao ya kijamii ni njia ya kushirikiana na kuelezea azma ya kuimarisha jamii.

XS
SM
MD
LG