Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 15, 2024 Local time: 08:29

Papa ahimiza ulimwengu kutonyamazia uadui na ukatili katika Pasaka yenye Vita


Papa Francis akitoa salaam za kheri ya Pasaka kwa jiji la Vatican na Ulimwengu kufikia mwisho wa ibada ya Pasaka ya Wakatoliki Jumapili katika viwanja vya mtakatifu Peter huko Vatican, April 17, 2022.
Papa Francis akitoa salaam za kheri ya Pasaka kwa jiji la Vatican na Ulimwengu kufikia mwisho wa ibada ya Pasaka ya Wakatoliki Jumapili katika viwanja vya mtakatifu Peter huko Vatican, April 17, 2022.

 Jumapili ya sikukuu ya Pasaka, Papa Francis amesema Yesu, mshindi dhidi ya dhambi, uoga na kifo, aliitaka dunia kutojisalimisha kwa uadui  na ukatili.

Alitoa wito huu wa dhati kwa ajili ya kutaka kumalizwa kwa vita Ukraine na kuwasihi waumini kuomba amani na kumalizika kwa ukatili na uharibifu usiokuwa na busara.

Kwa mikusanyiko ya watu wakati huu wa Pasaka ilikuwa ni kufufuka kwa kweli baada ya miaka miwili ya janga la corona ambalo lilifanya matukio Wiki Takatifu kusimamishwa.

Papa Francis ametoa wito wa nguvu kwa amani katika kile alichokiita “Pasaka ya vita.” Maelfu ya waumini walijitokeza katika siku yenye jua lakini upepo mwingi katika eneo la Mtakatifu Peter mwaka huu kuhudhuria ibada ya Pasaka, kusikiliza ujumbe wa papa na kupokea baraka zake.

Katika ujumbe wake [kwa jiji na dunia] Papa alihimiza amani kurejea katika nchi ya Ukraine iliyoko vitani, akielezea uchungu wa mtihani unaotokana na vita na uharibifu wa kikatili na vita visivyokuwa na busara. Francis ameutaka ulimwengu usizoee vita na kusema “huenda siku mpya ya matumaini itakuja haraka sana .”

Ni vyema upatikane uamuzi wa kufikia amani, Francis alisema, na kutanua misuli kumalizike wakati watu wanataabika. Alimsihi kila mtu kukubali kufikia amani kutoka katika roshani na mitaani na kuelezea matumaini kuwa viongozi wa mataifa mbalimbali watasikia kilio cha watu kuhusu amani.

Mawazo ya papa yalijikita kwa waathirika wengi wa vita huko Ukraine, mamilioni ya wakimbizi na watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi, familia zilizogawanyika, watu wazima walioachwa peke yao, maisha yaliyovunjika na miji iliyoharibiwa kabisa. Francis aliongeza kuwa katikati ya fmaumivu ya vita, kuna pia dalili zinazotia moyo, vitendo vingi vya ukarimu wakati familia na jamii wakifungua milango yao kuwakaribisha wahamiaji na wakimbizi kote Ulaya.

Katika Jumapili ya Pasaka waumini wanaadhimisha siku ya furaha zaidi katika kalenda ya Ukristo inayosheherekea kufufuka kwa Yesu siku tatu baada ya kufa akiwa msalabani.

Hivi leo kuliko wakati wowote mwingine, papa alisema, tunasikia sauti ikiakisi tangazo la Pasaka ambalo ni upendo wa Wakristo wa Mashariki: “Yesu amefufuka! Kwa ukweli amefufuka! Leo, kuliko wakati mwengine, ameongeza tunamhitaji, katika mwisho wa kpindi cha mateso kilionekana kuwa hakiishi.

Francis alisema mgogoro wa Ulaya ni lazima uifanye dunia iwe ina wasi wasi zaidi kuhusu hali nyingine za migogoro, kutaabika na majonzi, hali katika maeneo mengi ya dunia ambayo hayawezi kupuuzwa au kusahaulika.

Alizitaja Mashariki ya Kati, iliyoathiriwa na vita na mgawanyiko wa miaka mingi na hususan Libya, Yemen, Afghanistan na Myanmar. Papa pia amehimiza amani kwa bara zima la Afrika na kwa misaada kupelekwa kwa watu wanaotaabika kutokana na hali za kijamii huko Amerika ya Kati.

Francis alimaliza ujumbe wake wa Pasaka kwa maneno mazito: “Amani inawezekana, amani ni wajibu, amani ni jukumu kuu la kila mtu.”

XS
SM
MD
LG