India imechukuwa hatua kuiondolea Kashmir utawala wa ndani, jimbo ambalo linagombaniwa na nchi hizo mbili.
Bunge la Pakistan lilipitisha azimio Jumatano kulaani hatua ya India.
Bunge hilo pia limeitaka India iondoe vikwazo vyote ya kiusalama ilivyoiwekea Kashmir tangu Jumatatu.
Nchi jirani China na Pakistan ambazo zote zinadai eneo fulani la ardhi ya Kashmir limepinga vikali hatua ya india kuondoa madaraka ya kikatiba ambayo yanaruhusu Kashmir kutunga sheria zake yenyewe.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.