Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 06, 2023 Local time: 20:23

Operesheni dhidi ya wahamiaji katika kisiwa cha Mayotte yachochea mvutano


Eneo la makazi ya watu lenye umaskini katika Kisiwa cha Mayotte.

Serikali ya Ufaransa imetuma wanajeshi 2,000 na polisi kufukuza watu wengi, kuharibu makazi duni, na kutokomeza magenge ya kikatili katika kisiwa cha Mayotte chenye wahamiaji wengi.

Lakini operesheni hiyo imekuwa ngumu na kuibua wasiwasi wa unyanyasaji na kuzidisha mivutano kati ya wakaazi wa eneo hilo na wahamiaji kutoka nchi jirani ya Comoro.

Pia inaweka wazi umaskini katika jamii zote, mivutano juu ya hadhi ya kisiwa na ukosefu wa usawa kati ya Mayotte na Ufaransa yote.

Wakati Mayote ni sehemu ya Ufaransa , Comoro iko kilomita 100 kaskazini magharibi kupitia mlango wa Bahari ya Hindi pia lilikuwa koloni la Ufaransa lakini imekuwa huru tangu mwaka 1975.

Mayote ndio eneo maskini zaidi Ufaransa lakini mapato yake ya wastani ya kila mwaka ni karibu dola 3,500 ambayo bado ni mara mbili zaidi ya Comoro.

XS
SM
MD
LG