Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 12:51

Odinga bado adai uchaguzi haukuwa wa haki Kenya


Raila Odinga apiga kura kibra
Raila Odinga apiga kura kibra

Lakini Odinga na wanachama wa ushirika wa NASA wanasema kwamba uchaguzi uliibiwa kutoka kwao na kurudia msimamo wake huo mbele ya wafuasi wake waliokuwa na hamasa kubwa.

“Tumekuja kusema samahani, samahani, samahani kwa kile ambacho kimetokea hapa jana na siku nyingi,” amesema Odinga, “wanataka kuiba ushindi wetu, halafu wanakuja kuua watu wetu. Hiyo ndiyo kutokhofia kuchukuliwa hatua.”

Wakati huo huo, ofisi ya rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta inasema maandamano ya karibuni kote nchini kuhusu malalamiko ya uchaguzi yamekuwa na ghasia na kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press (AP), msemaji wa rais, Manoah Esipisu amesema Jumapili kwamba maandamano yoyote ya amani ni haki ya kikatiba na yatapewa ulinzi na polisi.

“Lakini cha kusikitisha maandamano yamekuwa ya ghasia, ambapo mali zimeharibiwa, na maisha ya watu yamekuwa hatarini,” amesema Esipisu na kuongezea ghasia zilikuwa kinyume cha sheria, kwahiyo ni vyema nielezewazi kuwa polisi hawatastahmili uvunjifu wa amani badala yake watalinda maisha ya watu na mali za wakenya.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema uchaguzi wa Jumanne uligubikwa na wizi. Tume ya uchaguzi imekanusha tuhuma hizo na kumtangaza rais Uhuru Kenyatta mshindi kuongoza awamu ya pili.

XS
SM
MD
LG