Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 22:47

Nigeria: Mahakama yaombwa kufuta Mashtaka dhidi ya matokeo ya uchaguzi


Bola Tinubu wa chama tawala cha APC, Nigeria alitangazwa kuwa mshindi  kwa asilimia 37.

Tume huru ya uchaguzi nchini Nigeria, INEC, imeiomba mahakama ya uchaguzi kufuta mashtaka dhidi ya matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Februari.

Bola Tinubu wa chama tawala cha APC alitangazwa kuwa mshindi kwa asilimia 37. Lakini wapinzania wake, Atiku Abubakari aliyeshika nafasi ya pili, na Peter Obi nafasi ya tatu, walikataa matokeo hayo na kupeleka mashtaka katika mahakama ya juu ya rufaa ya Nigeria.

Wanataka mahakama inayoshughulika na maswala ya uchaguzi kufuta matokeo ya uchaguzi wa rais. Katika utetezi wake, kwenye mahakama ya malalamiko ya uchaguzi wa rais, tume ya uchaguzi ilieleza maombi yaliyowasilishwa na wagombea wa upinzani kuwa hayana uwezo mkubwa na hayaeleweki kitaaluma.

Wafuasi wa chama cha Peoples Democratic Party (PDP) wakiandamana mbele ya makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Kitaifa (INEC) kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa February 25 mjini Abuja.
Wafuasi wa chama cha Peoples Democratic Party (PDP) wakiandamana mbele ya makao makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi ya Kitaifa (INEC) kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa February 25 mjini Abuja.

Awali INEC iliomba radhi kwa kuwepo matatizo ya kiufundi ambayo yalivuruga utaratibu wa kutoa matokeo ya uchaguzi kwa njia ya kielectroniki kutoka kwenye vituo vya uchaguzi.

ilisema kwamba kasoro zozote za matokeo kwenye tovuti yake na matokeo yaliyotolewa ana kwa ana yatafanyiwa uchunguzi na kutatuliwa.

Tume ya uchaguzi ilikosolewa na makundi ya waangalizi wa uchaguzi kwa kuwa na upungufu wa viwango vinavyohitajika.

XS
SM
MD
LG