Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 14:13

Netanyahu, Putin wajadili ugaidi Mashariki ya Kati


Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Waziri Mkuu wa Israeli amefanya ziara Moscow Alhamisi na kufanya mazungumzo na Rais wa Russia kuhusu mgogoro wa Syria.

Lakini wachambuzi wanasema hii ni dalili ya kuongezeka kwa ushawishi wa Russia Mashariki ya Kati na pia juu ya wasiwasi wa Isreali juu ya marafiki wa Moscow walioko Mashariki ya Kati.

Hata hivyo kitu kinachowatia wasiwasi maafisa wa Israeli ni uwepo mkubwa wa wapiganaji ndani ya Syria wenye mafungamano na Russia, wakiwemo maadui wa jadi wa Israeli; Iran na Hezbollah

Benjamin Netanyahu na Vladimir Putin hawakufanya mkutano na waandishi baada ya mazungumzo hayo, lakini Netanyahu baadae alitoa tamko kuwa “aliweka wazi” kwa Putin kwamba Israeli inataka kuzuia suala lolote la makubaliano ya Syria litaloipa “Iran na washirika wake nafasi ya uwepo wa kijeshi” huko Syria.

Russia imekuja kuchukua nafasi kubwa katika kukadiria sera ya nje ya Israeli kwa kuifanya itambue nguvu na ushawishi wake tangu Kremlin ilipoingilia kati mgogoro wa Syria September 2015.

Putin wakati huo aliweza kuhalalisha hatua iliochukuliwa na Russia wakati ilipoingia katika vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa na kikundi cha Islamic State, lakini wachambuzi wa nchi za Magharibi wanakataa kwa kusema kuingilia kati katika vita hiyo pia ilikuwa kuiokoa serikali ya rafiki wa Moscow iliyokuwa tayari imezingirwa, ambaye kiongozi wake ni Bashar al-Asaad.

Jukumu kubwa la Russia

Ni lile lengo la kuihami serikali ya Assad wengi katika nchi za Magharibi limewakera na ndio wanalokubali limefanikiwa-- hivi sasa.

Jukumu la Russia katika kuyasaidia majeshi ya Assad kuchukua mji wa Aleppo uliotekwa na waasi Disemba 2016, ilipelekea hatua muhimu ya kubadilika kwa vita hiyo.

Vikundi vya kujitegemea vya haki za binadamu vimesema ushindi huo uliweza kufikiwa kwa sababu ya mashambulizi ya kikatili ya anga yalifanywa kwa ushirikiano kati yaRussia na Syria yakiwalenga raia. Hata hivyo Russia imekanusha tuhuma hizo.

Israeli ilikaa mbali na mgogoro wa Syria, lakini iliendelea kushirikiana na Russia ilikuepusha uwezekano wa kutokea migongano na operesheni za kijeshi za Israeli katika mpaka wa Syria.

Israeli yaiangaza Iran

Na hasa Israeli inashtushwa vile inavyoonekana kwamba majeshi ya Iran yanaendelea kuchukua nafasi ya kudumu ndani ya eneo la mpakani la Golan Heights linaloshikiliwa na Israeli.

“Russia wamekuwa na mchango muhimu,” amesema Netanyahu katika tamko lake la kukiri juhudi za Russia katika kutokomeza maeneo ya kundi la Islamic State ndani ya Syria.

Amesema amemwambia kiongozi wa Russia “kama kawaida, hatutaki nafasi ya ugaidi uliopo ichukuliwe na utawala wa kigaidi wa msimamo mkali wa mashia unaoongozwa na Iran.”

XS
SM
MD
LG