Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:51

Mahakama ya Katiba South Korea 'yamtumbua' Rais Park


Wananchi wa Korea Kusini wakifurahia uamuzi wa Mahakama ya Katiba huko Seoul, Korea Kusini
Wananchi wa Korea Kusini wakifurahia uamuzi wa Mahakama ya Katiba huko Seoul, Korea Kusini

Mahakama ya Katiba nchini Korea Kusini imepiga kura kwa kauli moja kukubaliana na uamuzi wa kumuondoa madarakani Rais Park Guen-hye.

Kaimu Jaji Mkuu Lee Jung-mi ametoa maamuzi ya mahakama ya Katiba huko Seoul, Ijumaa ambayo yalitangazwa mubashara na vyombo vya habari vya taifa hilo.

“Tunaamini kuwa kunafaida nyingi kwa kumuondoa mshtakiwa katika wadhifa wake. Kwa hiyo kwa kura ya pamoja majaji wote tumetangaza kukubaliana na uamuzi wa kwanza uliofanywa na bunge wa kumuondoa rais madarakani. Mshtakiwa Rais Park Guen-hye ameondolewa madarakani.

Uamuzi ya Kumuondoa

Majaji wote nane wa Mahakama ya Katiba walipitisha uamuzi wa Bunge hilo, uliotolewa Disemba ukiungwa mkono na kura za wengi; theluthi mbili, ambao ulihitajika kupitisha uamuzi huo, ilikumuuzulu Park kutoka katika nafasi yake ya uongozi kutokana na tuhuma za ufisadi, uvunjaji wa sheria, na uzembe.

Mahakama imeelezea kuwa ni “uvunjaji wa sheria wa hali ya juu” wa katiba kutokana na madai kwamba Park alishirikiana na rafiki yake wa muda mrefu Choi Soon-sil kushawishi makampuni makubwa kuchangia zaidi ya dola milioni 69 kwa makampuni mawili yaliyokuwa yanashukiwa kuvunja sheria. Choi alikuwa anashutumiwa kuwa ana aina ya “nguvu ya ushawishi” juu ya Park na uwezo wa kuwadhibiti wafanyakazi wake, japokuwa hakuwa na jukumu rasmi la kiserikali.

“Uvunjaji wa sheria huu unadhoofisha utawala wa sheria na uwakilishi wa kidemokrasia,” amesema Lee.

XS
SM
MD
LG