Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 17:18

Ndugu wa hayati Desmond Tutu watoa salamu zao za mwisho


Kumbukumbu ya Wall of Remembrance katika Kanisa la St. Georges Cathedral, ukimuenzi Askofu Mkuu hayati Desmond Tutu, Cape Town, Disemba 27, 2021.(Photo by RODGER BOSCH / AFP).
Kumbukumbu ya Wall of Remembrance katika Kanisa la St. Georges Cathedral, ukimuenzi Askofu Mkuu hayati Desmond Tutu, Cape Town, Disemba 27, 2021.(Photo by RODGER BOSCH / AFP).

Ndugu wametoa heshima zao za mwisho kwa hayati askofu mkuu Desmond Tutu baada ya jeneza lililobeba mwili wake kuwasili katika kanisa la St Georges la Anglican mjini Cape Town.

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel ambaye kampeni zake zisizokuwa na woga zimeusaidia utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini kuleta demokrasia nchini humo, alifariki Jumamosi akiwa na umri wa miaka 90.

Jeneza lake litakuwepo katika Kanisa Kuu Alhamisi na Ijumaa ambapo watu wa kawaida wanakaribishwa kuuaga na kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kufanyika ibada kubwa siku ya mwaka mpya.

Wakati viongozi nchini Afrika Kusini wakiomboleza kifo cha shujaa huyo aliyepinga ubaguzi wa rangi, kaimu balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini Todd Hakel amezungumza na VOA kuhusu Wasifu wake.

Balozi alikuwa na haya ya kusema : “Nadhani katika uhai wake desmond tutu aliwavutia mamilioni ya watu kote duniani ikiwemo marekani. katika vita vyake kuhusu haki na pia wazo lake la watu kusimama na wanaokandamizwa , dhidi ya wakandamizaji, hakuna upande wowote. kati ya waliokandamizwa na wakandamizaji , ukichagua kutoegemea upande wowote , hakika uko Pamoja na dhalimu, nadhani ujumbe huo ulivutia mamilioni ya watu kote duniani lakini hata katika nchi yangu , kizazi changu, tuliona harakati za kupigania uhuru hapa Afrika kusini ni kitu ambacho kilituhamasisha wengiwetu katika huduma za umma, ikiwa pamoja na mimi mwenyewe. Kwa hakika askofu desmond tutu alikuwa sehemu kubwa ya hilo.”

XS
SM
MD
LG