Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 21:13

Nchi za Kiafrika zapiga hatua kutokomeza utapiamlo, udumavu


Mtoto akipimwa katika kituo cha Madaktari bila Mipaka (MSF), katika kijiji cha Nigeria.

Nchi za Kiafrika zimepiga hatua katika kumaliza utapiamlo na udumavu wa watoto lakini zinahitaji kufanya zaidi kufikia malengo ya utapiamlo yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa ifikapo 2025.

Huo ulikuwa ndio ujumbe mkuu wa mkutano ambao ulifanyika wakati wa Mkutano wa 33 wa Umoja wa Afrika.

Wasemaji kwenye mkutano wa Viongozi wa Kiafya wa Lishe (ALN) walijumuisha wakuu wa nchi za Madagaska, Cote d'Ivoire na Sierra Leone, mawaziri wa kitaifa wa afya pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB.org) Akinwumi Adesina.

Viongozi wamekiri ukubwa wa changamoto hiyo lakini walikuwa bado wanamatumaini. “Tunaweza kutokomeza njaa Afrika,” alisema Rais wa Madagascar Andry Rajoelina, moja wa viongozi watano wa Afrika wanaohamasisha lishe bora. “Natoa wito kwa wadau wenzetu wote kuendelea kufanya kazi nasi kukabiliana na njaa na utapiamlo.”

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara alisema viongozi lazima waliangalie suala hili kwa upana Zaidi. “NImependekeza AU iangaze katika kukabiliana na utapiamlo kama ni kauli mbiu ya 2021.

Tatizo la watoto wenye udumavu limepungua kwa asilimia nane katika bara la Afrika tangu mwaka 2000, ambayo ni hatua iliyopigwa kwa moja ya malengo ya Umoja wa Mataifa hadi kufikia 2025

Nchi za Kiafrika zimeonyesha kupiga hatua kubwa katika kufikia lengo la asilimia 50 la watoto ulimwenguni kuwa wananyonyeshwa maziwa ya mama zao bila ya kukosa kwa kipindi cha miezi sita tangu kuzaliwa.

Malengo mengine ni : kuzuia kuongezeka kwa unene; kupunguza ukosefu wa damu kwa wanawake wanao beba mimba; kupunguza watoto kuzaliwa na uzito wa chini na kupunguza uharibifu.

ALN, taasisi ambayo ni mshirika wa Umoja wa Afrika na Benki ya Maendeleo ya Afrika, imewaleta pamoja viongozi wa nchi, Mawaziri wa Fedha na viongozi wengine kuhamasisha kuongeza uelewa na kuwajibika, na serikali za Afrika kusaidia kuwekeza katika mradi huu ili kutokomeza utapiamlo kwa watoto.

Mkutano wa ALN, uliofanyika Addis Ababa Jumamosi, ulitoa fursa kutathmini mafanikio yaliyopatikana kabla ya Kilele cha mkutano wa Lishe kwa Ukuaji wa watoto utakaofanyika Tokyo, Japan, Disemba 2020.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG