Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 07, 2024 Local time: 13:36

Nchi tatu Afrika Magharibi zazindua chanjo ya Malaria kwa watoto


Akina mama wakisubiri watoto wao wapate chanjo huko Datcheka, Cameroon, Januari 22, 2024.
Akina mama wakisubiri watoto wao wapate chanjo huko Datcheka, Cameroon, Januari 22, 2024.

Benin, Liberia na Sierra Leone siku ya Alhamisi zimezindua mpango mkubwa wa chanjo unaojulikana Africa-focused initiative mpango unaotumainiwa kuokoa maisha ya maelfu ya watoto kila mwaka kote barani Afrika.

Nchi hizo tatu za Afrika Magharibi, ni za hivi karibuni kushiriki baada ya mafanikio ya kuanzishwa kwa utoaji chanjo wa kawaida ya malaria kwa watoto huko Kenya, Malawi, Burkina Faso, Cameroon, na Ghana, muungano wa kimataifa wa ushirika wa chanjo GAVI umesema katika taarifa.

Shirika la Afya Duniani limeidhinisha chanjo ambayo itafanyakazi pamoja na vifaa vilivyopo kama ya vyandarua ili kupambana na malaria, ambayo katika bara la Afrika kila mwaka inaua takribani nusu milioni ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.

“Uzinduzi huu… utasaidia kuokoa maisha na kutoa afueni kwa familia, jamii na mifumo ya afya iliyoelemewa,” amesema Aurelia Nguyen, afisa mkuu wa mipango wa GAVI.

Benin ina dozi ya chanjo 215,900 ambazo zitapatikana kwa watoto kuanzia umri wa miezi mitano, kulingana na GAVI

Sierra Leone ina dozi 550,000 na jirani yake Liberia ana dozi 112,000, imesema.

Katika uzinduzi rasmi huko Benin, uliofanyika katika mji wa Allada, kiasi cha kilometa 54 kutoka katika jiji kubwa la nchi hiyo Cotonou, watoto 25 walipatiwa chanjo.

Forum

XS
SM
MD
LG