“Ni siku ya kihistoria,” afisa mkuu wa Gavi kwa masuala ya chanjo Aurelian Nguyen, aliliambia shirika la habari la AFP katika kuadhimisha “hatua iliyopigwa” dhidi ya mapambano kwa ugonjwa huo. “tumekuwa tukifanyia kazi chanjo ya malaria kwa muda mrefu sana … miaka 30”
Ugonjwa wa maralia unasababishwa na vimelea vya mbu unaosambaa baada ya kung’atwa na mbu mwenye malaria. Mara nyingi watu huwa na dalili za mafua na kama haukutibiwa, unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwa ni pamoja na kifo.
Vituo vya kudhibiti magonjwa Marekani vimeripoti kwamba kulikuwa na takriban kesi milioni 241 za malaria kote dunaini katika kipindi cha mwaka 2020 na watu 627,000 walifariki dunia. Vifo vingi vilikuwa vya watoto barani Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara.
Chanjo mbili tofauti hivi karibuni zimeidhinishwa kwa ajili ya mapambano dhidi ya Malaria. Cameroon inatumia chanjo iliyotengenezwa na kampuni ya GlaxoSmithKline. Chanjo ya Chuo Kikuu cha Oxford ilitarajiwa kupatikana baadaye mwaka huu.
Chanjo zote mbili zinahitaji dozi kadhaa na hazizuii maambukizi. Maafisa wa afya wanawasihi watu kuendeleaa kutumia vyandarua, na kupuliza dawa za kuua wadudu katika kupambana dhidi ya Malaria.
Forum