Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 25, 2024 Local time: 22:49

Mahakama Kenya yaruhusu NASA kukagua mifumo ya IEBC


Viongozi wa NASA walipokutana na IEBC kabla ya uchaguzi
Viongozi wa NASA walipokutana na IEBC kabla ya uchaguzi

Mahakama ya juu nchini Kenya, Jumatatu imeamuru kwamba muungano wa upinzani wa National Super Alliance, NASA, uruhusiwe kukagua vifaa vya kielektroniki vilivyotumiwa wakati wa uchaguzi wa Agosti 8.

Katika uamuzi uliotolewa kwa kauli moja na majaji wote saba, mahakama hiyo imeitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC, kuwaruhusu mawakala wa aliyekuwa mgombea urais, Raila Odinga, kukagua mifumo ya kompyuta ili kuthibitisha matokeo ya uchaguzi huo wa rais.

Majaji hao aidha wameeleza kwamba kwa ripoti itakayotokana na hatua hiyo ya ukaguzi itakuwa ya manufaa kwa mahakama, kwa kuiwezesha kuelewa jinsi mifumo hiyo ilivyofanya kazi.

Hata hivyo, mahakama hiyo imekataa kuwaruhusu mawakala wa NASA, kuwa na uwezo wa kukagua mifumo hiyo bila udhibiti wowote, hali ambayo, imesema, itahakikisha kwamba hakuna hatari ya kudhuru mfumo wa kielektroniki uliotumiwa na tume hiyo.

Mahakama hiyo inaendelea kusikiliza kesi ambapo muungano wa NASA unapinga matokeo ya rais yaliyotangazwa na tume ya IEBC, kwamba rais Uhuru Kenyatta, alishinda.

XS
SM
MD
LG