Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 04:01

Lawama zadhoofisha juhudi za kuripoti mauaji ya Waislam wa Rohingya


Familia ambayo imewasili katika kambi ya wakimbizi nchini Bangladesh
Familia ambayo imewasili katika kambi ya wakimbizi nchini Bangladesh

Nadharia zinazotuhumu vyombo vya habari zimerudisha nyuma juhudi za waandishi kuripoti mgogoro wa Rohingya huko Myanmar, ambapo wengi wanaona kuwa zimeelemea upande moja zikiwakandamiza Wabuddha nchini humo.

Nadharia hizo ni pamoja na madai kuwa Waislam wanaushawishi zaidi katika shirika la habari la Uingereza BBC na Jumuiya ya nchi za Kiislam (OIC) ambayo inadaiwa kuwa inawalipa waandishi wa kigeni kuandika habari zile ambazo taasisi hiyo inataka kusikia.

Malalamiko hayo yanatokana na wasiwasi wenye ukweli wa kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikiangaza kwa kiwango kikubwa matatizo yanayowakabili Waislam wa Rohingya 400,000 ambao wamekimbia uvunjifu wa amani katika nchi ya Myanmar na madai ya mauaji ya kinyama ambayo wamekuwa wakisimulia huko walikokimbilia.

Matatizo yao yameweza kufika katika ngazi za juu za watawala wa dunia, ikiwa pamoja na kauli ya Makamu wa Rais wa Marekani Jumatano akieleza kwamba yale yanayojiri kuwa ni “maafa makubwa yanayo endelea kujitokeza”.

Kwa kulinganisha, wengi hapa wanajadili, kuwa waandishi – na halafu viongozi waliosoma habari hizo- wanapuuzia au kushindwa kutaja shambulizi la wapiganaji wa Arakan Rohingya Salvation Army, ambalo ndilo lililopelekea operesheni hiyo ya kijeshi, wakiwemo maelefu ya raia ambao sio Waislam ambao wamekimbia makazi yao, na vifo vya Wabuddha, Wahindu na makabila mengine madogo ambao walikuwa hawana hatia katika mgogoro huo.

Kwa hali yoyote kiongozi wa Myanmar Aung San Suu Kyi alieleza hisia hii katika sehemu ndogo ya hotuba yake juu ya mgogoro huu Jumanne, akisema “ wale waliolazimika kukimbia makazi yao ni wengi. Sio kwamba walikuwa Waislam peke yao na Wabuddha lakini pia makundi madogo kama vile Daing-net, Mro, Thet, Mramagyi na Wahindu ambao watu wengi hawana habari juu ya uwepo wao katika eneo hilo wanaloishi Waislam.”

XS
SM
MD
LG