Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:43

Raia wa Marekani kutumikia kifungo cha miaka 10 Iran


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson

Mahakama moja nchini Iran Jumapili imemhukumu mwanazuoni wa asili ya Kichina na Marekani kutumikia kifungo cha miaka 10 kwa tuhuma za ujasusi, kwa mujibu wa msemaji wa Mahakama hiyo.

Tangazo hilo lilipingwa mara moja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.

Xiyue Wang, mwenye umri wa miaka 37, mwenye uraia pacha wa China na Marekani, alikamatwa takriban mwaka mmoja uliopita, kwa mujibu wa mtandao wa Mizan, shirika la habari linaloendeshwa na mahakama ya Iran limeripoti.

“Serikali ya Iran inaendelea kuwashikilia raia wa Marekani na wengine wa kigeni kwa tuhuma za uongo zinazohusu usalama wa taifa,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema kwa tamko iliolitoa kwa vyombo vya habari.

“Tunataka raia wote wa Marekani waachiwe huru ambao wamezuiliwa bila haki huko Iran ili waweze kurejea kwa familia zao.”

Naibu mkuu wa Mahakama Iran, Gholamhossein Mohseni Ejeie, alitoa maelezo machache kuhusu kesi inayomhusu Xiyue Wang wakati akitangaza hatua hiyo ya mahakama Jumapili: “Mtu huyu alikuwa ametambuliwa na kukamatwa na vyombo vya usalama.

Mahakama hiyo imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka 10.” Hukumu hiyo inaweza kukatiwa rufaa.

Maafisa wa University ya Princeton wamemtambulisha Xiyue Wang kuwa mtafiti na mwanafunzi wa mwaka wa nne ambaye alikuwa anaandaa tafiti yake kwa ajili ya shahada ya uzamivu katika historia ya Asia na Ulaya ya mwisho wa karne ya 19 na mwanzoni mwa karne ya 20.

XS
SM
MD
LG