Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:03

Mwanasheria Mkuu wa zamani Kenya na familia wapigwa marufuku kuingia Marekani


Amos Wako
Amos Wako

Marekani imemweka aliyekuwa mwanasheria mkuu wa Kenya Amos Wako katika orodha ya watu waliopigwa marufuku kuingia Marekani kwa madai ya kuhusika katika rushwa.

Kulingana na taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Marekani, Wako, pamoja na mkewe Flora Ngaira na mwanawe Julius Wako, wamepigwa marufuku kuingia Marekani.

Serikali ya Marekani inasema hatua hiyo imechukuliwa kutuma ujumbe kwamba Marekani inashirikiana na Kenya katika kupambana na rushwa.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaelezea waziwazi ni vitendo gani vya rushwa Wako alihusika navyo.

Wako alikuwa mwanasheria mkuu wa Kenya kwa muda wa miaka 20, kati ya mwaka 1991 na 2011.

Amos Wako kwa sasa ni seneta wa Kaunti ya Busia, magharibi mwa Kenya na vyombo vya habari vya Kenya vimemhusisha na nia ya kutaka kugombea nafasi ya gavana katika Kaunti hiyo.

XS
SM
MD
LG