Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 18:56

Mwanasheria Mkuu Uganda apinga Mkuu wa Jeshi, Spika kuhojiwa


Wabunge wa Uganda wakipigana makonde Bungeni September 26, 2017.
Wabunge wa Uganda wakipigana makonde Bungeni September 26, 2017.

Waliowasalisha kesi hiyo pia wanapinga hatua ya Bunge hilo kuongeza muda wa rais na wabunge kutumikia wadhifa huo kutoka miaka 5 hadi 7.

Jopo la majaji watano wakiongozwa na Jaji Mkuu Alphonse Owiny Dollo inasikiliza ombi la kupinga hatua ya Bunge la Uganda kuifanyia mabadiliko ibara ya 102(b) ya Katiba ya nchi hiyo, kuhusu umri wa wagombea urais.

Kesi hiyo inasikilizwa katika mji wa Mbale, kilomita 200 mashariki mwa mji wa Kampala.

Kikao cha leo kimekuwa cha kutoa mwelekeo jinsi kesi hiyo itakavyoendeswa na wale watakaoshirikishwa.

Masuala 13 kusikilizwa

Kati ya masuala 13 yanayosikilizwa ni pamoja na hatua ya kuwasilishwa kwa muswada uliopelekea katiba kufanyiwa marekebisho, iwapo ulifanyika kwa mujibu wa sheria.

Kwa sababu kuna madai kwamba wakati wa kuwasilishwa kwake, kiongozi wa upinzani hakuwepo bungeni na wabunge wa upinzani walifukuzwa na spika.

Mahakama ya katiba pia inatakiwa kuamua iwapo hatua ya wanajeshi kuingia bungeni na kuwacharaza wabunge viboko na kuwapiga ngumi wakati wa kuwasilishwa muswada wa mabadiliko hayo ya sheria haukuwa kinyume cha sheria.

Je mchakato ulifuata sheria?

Pande husika pia zitaangalia mchakato mzima uliofuatwa katika kuifanyia Katiba hiyo marekebisho, ikiwemo kuandikwa kwa muswada huo, kutafuta maoni ya raia, kujadili na kupitishwa kwake.

Wanaowasilisha kesi hiyo wanadai kwamba chama kinachotawala cha National Resistance Movement (NRM), hakikuwashirikisha raia katika kufanya mabadiliko hayo na kwamba mchakato mzima uligubikwa na fujo.

Mahakama pia inatakiwa kueleza iwapo Bunge lilitii sheria kwa kuifanyia katiba marekebisho kuhusu utawala wa nchi badala ya kuruhusu raia kufanya uamuzi kupitia kwa kura ya maoni.

Mawakili wanataka mahakama kumwamrisha Mkuu wa Jeshi la Uganda Jenerali David Muhoozi na Spika wa Bunge Rebecca Kadaaga kufika mahakamani ili kuhojiwa.

Lakini Mwanasheria Mkuu Mwesigwa Rukutana, amepinga ombi hilo akisema kwamba maafisa wote wa ngazi ya juu serikalini wanakingwa na sheria na hawawezi kufika mahakamani kuhojiwa.

Muungano wa mawakili

Walalamikaji, wakiongozwa na muungano wa mawakili nchini Uganda na wabunge sita wa upinzani, wanasisitiza kwamba ni ukiukwaji wa katiba kwa wabunge kujiongezea muda wao katika nafasi za ubunge kutoka miaka 5 hadi 7.

Mnamo tarehe 20 mwezi Disemba 2017, Bunge la Uganda lilifanya marekebisho ya katiba ya nchi hiyo na kuondoa kikomo cha umri kwa wagombea urais, pamoja na kuongeza mda wa sasa wa rais na wabunge ofisini kutoka miaka 5 hadi 7.

Wachambuzi wa siasa wanasema kwamba hatua hiyo inamnufaisha rais wa sasa Yoweri Museveni ambaye katiba ilikuwa inamzuia kugombea tena urais baada ya kuitawala nchi hiyo kwa kipindi cha miaka 35.

Majaji wana muda wa siku 7 kusikiliza kesi hiyo kabla ya kufanya maamuzi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Kennes Bwire, Washington, DC

XS
SM
MD
LG