Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 30, 2020 Local time: 08:17

Mwanafunzi afariki katika chuo kikuu Nairobi


Wanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi watoa damu kusaidia wenzao waliojeruhiwa katika mkanyagano Aprili 12, 2015

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Nairobi huko Kenya amefariki dunia Jumapili kufuatia mkanyagano wa wanafunzi waliokuwa wakitoroka baada ya mlipuko mkubwa wa mtambo wa umeme,uliodhaniwa kuwa shambulizi.

Wanafunzi waliojawa na wasiwasi katika chuo kikuu cha Kikuyu ambacho ni sehemu ya chuo kikuu cha Nairobi, walidhania mlipuko huo ni shambulizi la wanamgambo wa al-Shabab ambao majuzi walishambulia wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa na kuuwa wanafunzi 148.

Zaidi ya wanafunzi 100 walijeruhiwa katika mkanyangano huo mapema Jumapili. Baadhi yao waliruka kutoka orofa ya tano kupitia madirisha, wakijaribu kutoroka chuo wakidhania wamevamiwa na magaidi.

Vyombo vya habari vya Kenya vinaripoti kuwa baadhi ya wanafunzi walipata majeraha mabaya.

Ona maoni (2)

mjadala huu umefungwa

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG