Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 22:32

Mwanadiplomasia wa China aitaka BRICS kuungana kukabiliana na fikra za vita baridi


Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi

Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu ameitaka BRICS kuungana wakati ikikabiliwa na fikra za vita baridi

Waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi ametoa wito huo wa kuimarisha umoja na ushirikiano kati ya nchi wanachama wa BRICS, wakati kuna changamoto za kisiasa alizodai zinatokana na fikra za vita baridi.

Akizungumza katika mkutano wa 14 wa maafisa wa usalama wa ngazi ya juu wa BRICS huko St. Petersburg, Wang amezungumzia ukosoaji wa baadhi ya nchi, unaoelekezwa kwa muungano huo.

Ametoa wito kwa nchi wanachama kulinda maslahi yao, kutatua tofauti, kulinda uhuru wao na kujenga maslahi.

Mkutano huo umefanyika kabla ya mkutano mkuu wa viongozi wa nchi wanachama wa BRICS utakaofanyika Kazan, ambapo rais wa Russia Vladimir Putin na mwenzake wa China Xi Jinping wanatarajiwa kuhudhuria.

Rais wa China akiwa na viongozi wa baadhi ya nchi za Afrika katika mkutano wa BRICS Agost 24, 2023. Picha na REUTERS/Alet Pretorius
Rais wa China akiwa na viongozi wa baadhi ya nchi za Afrika katika mkutano wa BRICS Agost 24, 2023. Picha na REUTERS/Alet Pretorius

BRICS ni muungano ulioanzishwa mwaka 2006 unaozileta pamoja Brazil, Russia, India, China na Afrika kusini.

Nchi wanachama wameongezka na kujumuisha Iran, Misri, Ethiopa na Umoja wa Falme za Kiarabu. Saudi Arabia inatarajiwa kujiunga huku Azerbaijan, Uturuki na Malaysia zikiwa zimetuma maombi ya kujiunga.

Forum

XS
SM
MD
LG