Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:26

China haikutoa afueni ya madeni Afrika lakini imeahidi kutoa dola bilioni 50


Mkutano wa ushirikiano kati ya China na Africa (FOCAC) mjini Beijing.
Mkutano wa ushirikiano kati ya China na Africa (FOCAC) mjini Beijing.

China imetaka kutumia FOCAC kukabiliana na ukuaji wa ushindani katika Afrika kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya na Japan.

China haikutoa afueni ya madeni iliyoombwa na nchi nyingi za Afrika wiki hii, lakini iliahidi kutoa dola bilioni 50.7 kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitatu katika mikopo na uwekezaji.

Mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliozinduliwa mwaka 2000 uliangazia jukumu lililoimarishwa baada ya kuanzishwa mwaka 2013 kwa Mpango wa Rais Xi Jinping wa juhudi za ujenzi wa miundo mbinu maarufu kama BRI, ambao unalengo la kuzikarabati barabara za zamani katika bara hilo.

China inarudi kwenye mstari wa mbele kwa haraka katika misingi ya upelekaji mitaji nje ya nchi katika masoko yanayoibukia, alisema Hasnain Malik wa Tellimer, huku akiongeza kuwa bado haijafikia katika viwango vya kabla ya COVID.

China pia imetaka kutumia FOCAC kukabiliana na ukuaji wa ushindani katika Afrika kutoka Marekani, Umoja wa Ulaya, Japan na wengineo.

Forum

XS
SM
MD
LG