Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 06:14

Nassari ambana Mwakyembe Bungeni Dodoma


Waziri Mwakyembe
Waziri Mwakyembe

Kashfa ya Richmond imeibuka tena ndani ya Bunge la Taifa nchini Tanzania ambako kulikuwa na malumbano makali kati ya Waziri na mbunge wa chama cha Upinzani.

Mvutano huo ulitokea wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dr Harrison Mwakyembe Alhamisi alipowataka wabunge wa upinzani kulirudisha suala la Richmond Bungeni kwa mara nyingine.

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa wakati akifanya majumuisho ya makadirio ya bajeti ya 2017/2018 kwa ajili ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) na yale ya Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Mwakyembe alisisitiza kuwa Kamati Teule ya Bunge ilifanya uchunguzi kwa haki na kwa weledi mwaka 2008.

Waziri Mwakyembe alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) kumbana waziri huyo Jumatano jioni kwa madai ya kukosekana uadilifu.

Mbunge huyo alidadisi msimamo wa serikali katika kuendeleza utawala bora, akisema ni mawaziri wa serikali hiyo ndiyo wenye kukiuka maadili kwa kuonesha upendeleo.

Kamati hiyo ilichunguza kashfa ambayo ilipelekea kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ambaye hivi sasa amejiunga na chama cha jupinzani cha Chadema.

XS
SM
MD
LG