Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 01:42

Museveni aomba Kenya msamaha


Generali Muhoozi Kainerugaba, mwanawe rais wa Uganda Generali Yoweri Museveni. PICHA: AFP
Generali Muhoozi Kainerugaba, mwanawe rais wa Uganda Generali Yoweri Museveni. PICHA: AFP

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameomba Kenya msamaha kutokana na ujumbe wa mwanawe Muhoozi Kainerugaba kwamba jeshi la Uganda linaweza kudhibithi Nairobi kwa rahisi sana katika mda wa wiki mbili.

Generali Muhoozi Kainerugaba vile vile alisema kwamba ni aibu kwamba Kenya inadai kuheshimu mfumo wa demokrasia na katiba, jambo ambalo haliwezi kukubalika Uganda, akisema kwamba “rais mstaafu Uhuru Kenyatta angegombea mhula wa tatu kama angetaka kufanya hivyo, badala ya kufuata katiba ya nchi.”

Aliendela kuandika kwamba Kenya inastahili kuwa chini ya Uganda kama njia ya ukombozi.

Ujumbe wa Muhoozi ulizua majibizano makali kwenye mtandao wa twiter kutoka kwa Wakenya, na baadaye wizara ya mambo ya nje ya Uganda kuandika taarifa ikijitenga na ujumbe wa Muhoozi, ikisisitiza kwamba maswala ya uhusiano wa kimataifa hayafanyiki kwenye mitandao ya kijamii na kwamba aliyoandika Muhoozi sio msimamo wa Uganda bali fikira zake za kibinafsi.

Ombi la msamaha

Museveni ametuma taarifa kwa vyombo vya habari na pia kuchapisha kwenye mtandao wake wa Twiter, akisema kwamba “naomba ndugu zetu wa Kenya kutusamehe kutokana na ujumbe alioandika Generali Muhoozi kuhusiana na uchaguzi wa Kenya.”

Museveni alipandisha cheo Kainerugaba saa chache baada ya majibizano yake na wakenya kwenye twiter na kuwa General.

Kabla ya mabadiliko hayo katika jeshi, Muhoozi alikuwa Luteni generali na kamanda wa majeshi ya nchi kavu.

Na baada ya kupandishwa cheo, alituma tena ujumbe mara kadhaa akimpongeza babake kwa kumwamini katika majukumu anayompa na kumpandisha madaraka.

Museveni amesema kwamba “sio sahihi kwa watumishi wa uma, hasa wanajeshi kuzungumzia au kuingilia maswala ya nchi nyingine,” akiongezea kwamba “ njia pekee inayokubalika ni kupitia kwa mchakato uliopo wa umoja wa Afrika au jumuiya ya Afrika mashariki.”

Mbona kupandishwa cheo baada ya ‘kukosea’?

Ametetea hatua yake ya kumpandisha cheo Muhoozi baada ya kujibizana na wakenya kwenye twiter akisema kwamba “kuna mambo mengi mazuri ambayo amefanya katika jeshi na kuna mengi anayoweza kufanya. Hatua yangu ni yza kuzuia mabaya na kutoa fursa ya kufanya mema, akisisitiza kwamba “nasikitika sana ndugu zetu wakenya, naomba pia msamaha kwa wanajeshi wa Uganda ambao huenda walikasirishwa na hatua ya mmoja wao kwa kuingia maswala ya Kenya.

Museveni hata hivyo amesisitiza kwamba “najua vizuri sana bila shaka yoyote kwamba Muhoozi ni mtu anayependa sana Afrika na anataka maendeleo Afrika.”

XS
SM
MD
LG