Steve Stephens anadaiwa kumpiga risasi na kumuua mtu mzima mmoja huko Cleveland, Ohio, aliweka video ilionyesha mauaji hayo katika mtandao wa Facebook wakati wa sikukuu ya Easter Jumapili na baadae kujaribu kuwakimbia polisi.
Polisi wa Jimbo la Pennsylvania wamesema kupitia Twitter, maafisa wa polisi walimtia machoni Stephens katika Kaunti ya Erie Jumanne asubuhi.
“Baada ya kumkimbiza kwa muda mfupi, Stephens alijipiga risasi na kujiua yeye mwenyewe,” polisi wamesema.
Stephens alikuwa katika orodha ya watu wanaotafutwa sana na polisi na kulitolewa zawadi ya dola 50,000 kwa mtu atayeweza kutoa taarifa zake zitazowezesha kukamatwa kwake.
Stephens inadaiwa alichukua picha yake wakati anafanya mauaji na kuiweka video hiyo katika Facebook pamoja na video nyingine ambazo anadai alihusika kipindi cha nyuma na kuwaua watu wengine 13.
Polisi waliokuwa wanamchunguza Stephens, hata hivyo, wanasema hawajapata ushahidi wowote unaoonyesha kwamba kweli aliwaua watu wengine 13.
Katika mahojiano na shirika la televisheni la CNN, mama yake Stephen amesema mwanawe alimwambia alimuua mtu huyo kwa sababu “alikuwa amekasirishwa na mpenzi wake.”
Polisi wamesema kuwa mhanga huyo aliyeuawa alikuwa anafanya kazi za uunzi na alikuwa na watoto 10. Alikuwa akikusanya makopo ya aluminium pembeni ya barabara wakati ambapo Stephen akipita na gari lake na kumpiga risasi.