Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:57

Tanzania yamshikilia mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari


Wahanga wa mauaji ya kimbali
Wahanga wa mauaji ya kimbali

Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Innocent Sagahutu amepelekwa makao makuu ya uhamiaji mkoani Dar es Salaam kwa ajili ya mahojiano.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi nchini Tanzania Sagahutu alikamatwa hivi karibuni eneo la mpakani wilayani Ngara alipokuwa akielekea Burundi.

Akizungumzia tukio hilo Jumanne, ofisa uhamiaji mkoa wa Kagera Abdallah Tiwo alisema mtuhumiwa huyo amepelekwa makao makuu kwa ajili ya uchunguzi.

"Ni kweli alikuwa anashikiliwa na uhamiaji mkoa wa Kagera, ila sasa anaelekea Dar es Salaam makao makuu ya uhamiaji," alisema.

XS
SM
MD
LG