Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 01:36

Mtu mmoja achomwa kisu na 10 wakamatwa Washington, DC


Wafuasi wa Rais Donald Trump wakikusanyika mjini Washington, D.C. Jumamosi, mchana.
Wafuasi wa Rais Donald Trump wakikusanyika mjini Washington, D.C. Jumamosi, mchana.

Mtu mmoja amechomwa kisu na wengine 10 wamekamatwa baada ya ugomvi kuzuka mjini Washington, DC Jumamosi usiku kati ya wafuasi wa Rais Donald Trump na waandamanaji wanaompinga.

Fujo hizo zilizuka baada ya maadamano katikati ya mji wa Washington yaliyo itishwa na makundi mbali mbali ya mrengo wa kulia na kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa Trump, wakirudia madai yake ya wizi wa kura yasiokuwa na uthibitisho.

Kwa mujibu wa msemaji wa idara ya zimamoto ya jiji na huduma za matibabu ya dharura, mtu aliyechomwa kisu alifikishwa kituo cha afya.

Gazeti la Washington Post limeripoti kuwa shambulizi hilo la kisu lilitokea wakati wa vurugu kati ya wafuasi wa Trump, baadhi yao wakiwa wamebeba virungu, na waandamanaji wanaompinga zilizotokea majira ya saa mbili usiku.

Idara ya polisi ya jiji la Washington imewakamata watu 10 mpaka jana mchana, msemaji amewaambia waandishi, wakiwemo wanne kwa uvunjifu wa sheria ya kubeba silaha, wawili kwa shambulizi na mmoja kwa kumshambulia afisa wa polisi.

Maelfu ya wafuasi wa Rais Donald Trump waliandamana katikati ya mji wa Washington Jumamosi kuendelea kuunga mkono madai yake yaliokuwa hayajathibitishwa ya wizi wa kura wakati akiendelea kushinikiza kupinga kisheria matokeo ili kubatilisha ushindi wa matokeo ya Rais mteule Joe Biden.

Biden kwa upande wake ameendelea kujizatiti katika ushindi wake Ijumaa wakati matokeo kutoka kituo cha Utafiti cha Edison kikionyesha ameshinda Georgia, na kumwezesha kuwa na jumla ya kura za wajumbe 306 ikiwa inapita idadi inayohitajika ya 270 kuchaguliwa kuwa rais na Trump kujipatia kura za wajumbe 232.

Kura hizo 306 ni sawa na kura alizopata Trump mwaka 2016 kumshinda Hillary Clinton, ambazo wakati huo aliziita “ushindi wa kishindo.”

XS
SM
MD
LG