Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 04:54

Viongozi waangazia diplomasia kufuatia ushindi wa Biden


Viongozi mbalimbali duniani wanaendelea kutuma ujumbe wa pongezi kwa rais mteule wa Marekani Joe Biden baada ya matokeo ya awali yanaonyesha kwamba ameshinda uchaguzi mkuu wa urais uliondaliwa iki iliopita.

Lakini China na Russia zimesalia kimya zikisubiri maamuzi ya mahakama.

Barani Ulaya, sherehe kubwa zilifanyika Ballina, Ireland, licha ya watu katika nchi hizo kuwa chini ya masharti makali ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Corona. Ukoo wa Biden unaanzia Ireland.

Mara nyingi, Biden amezungumzia fahari ya ukoo wake nchini Ireland. Ameonya Uingereza kwamba kujiondoa kwake katika umoja wa ulaya haustahili kuathiri amani kaskazini mwa Ireland.

Mwaka uliopita, Biden alimtaja waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson kuwa sehemu ya Donald Trump.

Kauli ya Boris Johnson

Boris Johnson alisema jumapili kwamba yupo tayari kufanya kazi na utawala mpya wa Marekani.

“Nadhani kwamba kuna mambo mengi sana yanayounganisha serikali ya nchi hii na serikali ya Marekani, wakati wowote kwa awamu yoyote, kuliko yale yanayotutenganisha.” Alisema Johnson.

Umoja wa ulaya umekaribisha ushindi wa Joe Biden.

“Tutashirikiana kutatua changamoto zinazosumbua ulimwengu kama janga la virusi vya Corona, kudorora kwa uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa, utawala bora, uchumi wa kidigitali na jamii, usalama na mifumbo mbalimbali.” Amesema rais wa tume ya umoja wa ulaya Ursula Von der Leyen.

Matarajio ya ulaya

Lakini mchambuzi Inderjeet Parmar, wa chuo kikuu cha City mjini Londona, anasema kwamba bara la ulaya lisiwe na matarajio makubwa na rahisi.

“Kutokana na mazingira yenye ushindani mkubwa, nadhani kwamba Marekani itaendelea na msimamo wake mkali. Mikataba ya biashara na ulaya na Uingereza haitakuwa rahisi. Nadhani pia kwamba muungano wa NATO utahtaji nchi za ulaya kuajibika Zaidi.”

Kansela wa Ujerumani Angela Markel ameonekana kukiri kwamba kutakuwepo changamoto hizo.

“Marekani inasalia kuwa mshirika wetu muhimu sana lakini inatarajia kwamba tutaendelea kuimarisha usalama wetu.”

Mkataba wa nuclear na Iran

Nchi za ulaya zina matumaini kwamba Joe Biden atatafuta njia ya kurudisha Marekani katika mkataba wa nuclear na Iran.

Israel inapinga sana hatua hiyo. Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, katika ujumbe wa video wa kumpongeza Biden, hakuzungumzia mkataba huo, lakini alisema kwamba anamjua Biden kama Rafiki mkubwa wa Israel.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, ameandika kwa twitter kwamba Trump ataondoka katika mda wa siku 70 lakini Iran itabaki daima, akiongezea kwamba sio jambo jema kutegemea watu wengine kutoa ulinzi kwa taifa la wengine. Amesema kwamba Iran ipo tayari kwa mazungumzo na majirani, kutatua migogoro.

Televisheni ya serikali ya China, ambayo ipo katika mgogoro wa kibiashara na Marekani, imesema kwamba ushindi wa Biden unatoa fursa ya ubashiri Zaidi.

Imeyatarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG