Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:18

Inamaanisha nini kuwa Rais Mteule nchini Marekani


Rais mteule wa Marekani Joe Biden
Rais mteule wa Marekani Joe Biden

Nchini Marekani, Mdemokrat Joe Biden anatajwa kuwa rais mteule.

Rais mteule ni maelezo na siyo nafasi rasmi ya madaraka. Ilivyokuwa Biden hana madaraka katika serikali, na hatokuwa na madaraka mpaka atakapo apishwa mchana wa Januari 20, 2021.

Mitandao ya habari ya Marekani, inayofuatilia zoezi la kuhesabu kura, ilikadiria Novemba 7 kuwa kuongoza kwa Biden katika kura kusingeweza kushindwa huko Pennsylvania, na kumwezesha kupata kura za wajumbe zaidi ya 270 zinazohitajika kushinda urais. Ndani ya dakika kadhaa za kuthibitisha anaongoza hesabu hizo zilikuwa hazina shaka, na kutajwa atakuwa mshindi.

Ndio maana vyombo vya habari, ikiwemo VOA, wanamwita Biden kuwa “ametajwa kuwa ni mshindi wa urais.”

Wakati mwengine, inapotokea uchaguzi uliokaribiana, mitandao ya habari inapotangaza matokeo, mgombea mwengine hatokubali kushindwa.

Rais Trump na Rais mteule Joe Biden
Rais Trump na Rais mteule Joe Biden

Rais Donald Trump hajafanya hivyo, akidai kuwepo wizi wa kura bila ya ushahidi wa kutosha na kuapa kupigania hilo.

Msimamo wa rais umewaacha wabunge huko Washington wakiwa wamegawanyika, ambapo Warepublikan wanaunga mkono uchunguzi wa kisheria juu ya madai ya wizi wa kura, hata pale ambapo wao wanaendelea kusheherekea ushindi wa wabunge wengine wa Bunge la Marekani katika uchaguzi huohuo.

Lini suluhu itapatikana juu ya mgogoro huu?

Uchaguzi wa Marekani hautathibitishwa rasmi kwa wiki kadhaa. Wakati huu, kesi za kisheria na majimbo kuhesabu tena yanaweza kutokea.

Hadi sasa, uongozi wa Trump haujatoa ushahidi wa wizi wa aina yoyote ambao unaweza kubadilisha matokeo, lakini bado kuna muda wa kupinga kisheria matokeo.

Mara kura zitakapo thibitishwa na majimbo, wajumbe waliokula kiapo watapiga kura zao ifikapo katikati ya mwezi Disemba. Bunge baada ya hapo linapitisha matokeo ya kura za wajumbe ifikapo mapema Januari, wiki mbili kabla ya kuapishwa rais.

XS
SM
MD
LG