Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 02, 2022 Local time: 15:51

Mtu ajiua mbele ya Ikulu ya White House, asababisha taharuki


Rais Donald Trump na mkewe wakirejea Wakiwasili Ikulu ya White House

Mtu mmoja ametumia bunduki kujiua Jumamosi karibu na Ikulu ya White House jijini Washington, Marekani walinzi wa ikulu ya rais wamesema.

Mwanaume huyo alikuwa karibu na wigo wa Ikulu katika barabara ya Pennsylvania na kuchomoa bunduki na kurusha risasi hewani mfululizo.

Hata hivyo taarifa za ikulu zimeripoti kuwa Rais Donald Trump hakuwa kwenye Ikulu. Wakati wa tukio hili alikuwa katika jumba lake la kifahari la Mar-a-Lago katika jimbo la Florida.

Pia katika tukio hilo hakuna mtu aliyejeruhiwa, kwa mujibu wa vyombo vya usalama.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema wakati mtu huyo anarusha risasi kulikuwa na msongamano wa watu.

Picha ya video kwenye mtandao wa Twitter ilionyesha jinsi tukio hilo lilivyo sababisa taharuki kati eneo hilo na kusababisha watu kusambaratika na kutafuta eneo la kujificha.

Polisi hadi tunachapisha habari hizi walikuwa hawajataja jina la mtu aliyehusika na utumiaji wa silaha katika eneo la ikulu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG