Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 21, 2024 Local time: 07:17

Mshukiwa wa mauaji ya watu sita Atlantą akamatwa


Polisi wakiwa nje ya jengo ambako mauaji yalitokea.
Polisi wakiwa nje ya jengo ambako mauaji yalitokea.

Maafisa wa usalama wa jimbo la Georgia Marekani wamesema wamemkamata mwanaume mmoja anayeshukiwa kuwapiga risasi na kuwaua watu wanane, sita kati yao wakiwa ni wanawake wa asili ya Asia.

Mashambulizi hayo yalitokea Jumanne. Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini imesema kuwa wanne kati ya waliouawa walikuwa wenye asili ya Korea.

Shambulizi la kwanza lilitokea katika jengo la biashara lililo katika mji wa Acworth, takriban kilomita 50 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo, Atlanta, ambapo, kwa mujibu wa mamlaka, watu wanne waliuawa.

Saa moja baadaye polisi mjini Atlanta waliwapata wanawake watatu wa asili ya Korea wakiwa wameuawa kwa kupigwa risasi ndani ya jengo lilokuwa na biashara ya saluni, na mwili wa mwanamke mwingine kupatikana karibu na eneo hilo.

Polisi wamesema walifukuzana na mshukiwa, Robert Aaron Long, mwenye umri wa miaka 21, ambaye alikuwa akiendesha gari lake, na hatimaye kumtia mbaroni, takriban kilomita 240, kusini mwa mjia wa Atlanta.

Mashambulizi hayo yanajiri wakati ambapo hali ya taharuki imeendelea kupanda katika sehemu mbalimbali hapa Mrekani, kufuatia ongezeko la mashambulizi yanayolenga watu wa asili ya Asia.

Matukio hayo yamekuwa yakilaaniwa vikali na baadhi ya wanasiasa, na viongoizi wa jamii zilizo na wakazi wengi kutoka bara Asia.

XS
SM
MD
LG