Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 27, 2022 Local time: 23:30

Mshukiwa wa mauaji ya Florida kufikishwa mahakamani


Nikolas Cruz (kushoto) akifikishwa mahabusu baada ya kukamatwa katika tukio la mauaji Florida.

Mtu ambaye anaonekana kuwa alikuwa na matatizo anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kutumia bunduki Marekani ambaye inatarajiwa kuwa atafikishwa mahamani kwa mara ya kwanza Alhamisi.

Vyombo vya usalama vimemfungulia mashtaka 17 Nikolas Cruz ya kukusudia kuua baada ya kudaiwa kuwa aliwamiminia risasi wanafunzi na waalimu kwa kutumia bunduki ya kivita Jumatano katika shule ya sekondari ya South Florida ambako aliwahi kuwa mwanafunzi na baadae kufukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Polisi walimkamata Cruz nje ya shule ya sekondari Marjory Stoneman Douglas huko Parkland, kiasi cha kilomita 70 kaskazini ya mji wa Miami.

Polisi wamesema kuwa Cruz, akiwa amevaa kifaa cha kuzuia gesi, alianza kupiga bunduki nje ya shule na kuendelea kupiga bunduki ndani ya jengo na hatimaye kujichanganya na wanafunzi wakati wakikimbia.

Habari zaidi zinasema mbali ya vifo 17 vilivyoripotiwa na polisi, shambulizi hilo limewajeruhi wengine 15.

Mkuu wa polisi wa Kaunti ya Broward Scott Israel amewaambia waandsihi wa habari kuwa mshambuliaji huyo alikuwa na magazini zenye risasi nyingi na aina ya bunduki AR-15.

Vyombo vya usalama vimeongoza kuwa alinunua silaha hizo kisheria mwaka moja uliopita baada ya kufanyiwa uchunguzi wa maisha yake.

Vyombo vya usalama havijatoa maelezo ya papohapo kuhusiana na mauaji yaliyojiri wakati wa kumalizika muda wa masomo siku hiyo ya tukio iliyokuwa na jua kali.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG