Mkuu wa polisi wa wilaya ya Broward, Scott Israel alieleza kwamba ilikuwa siku ya maafa mabaya kwa wilaya yake na kumtaja jina mtuhumiwa kwa shambulizi hilo la kikatili kuwa ni Nicolas Cruz.
Polisi walieleza mtuhumiwa alikamatwa nje ya uwanja wa shule bila ya kupambana. Mkuu wa polisi alisema Cruz alikua na risasi nyingi na bunduki mmoja. Israel anasema waaathirika 12 walifariki ndani ya shule, wengine watatu waliuliwa nje ya majengo ya shule na wawili walifariki kutokana na majeraha huko hospitali. Pia kuna watu wengine 14 waliojeruhiwa.
Rais wa Marekani, Donald Trump ameahidi kutoa msaada kwa wakuu wa Florida ili kusaidia katika maafa hayo yaliyotokea.