Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 22:39

Msanii Roma Mkatoliki ahojiwa kituo cha polisi


Kamanda Simon Sirro
Kamanda Simon Sirro

Msanii Roma Mkatoliki wa Tanzania amepatikana na yupo Kituo cha Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam akihojiwa pamoja na wenzake.


Vyanzo vya habari nchini Tanzania vinasema kuwa kupatikana kwa Roma kumethibitishwa pia na Mkurugenzi wa Tongwe Records J. Mada.

Lakini hata hivyo bado hakuna maelezo ya kutosha kuhusiana na wapi alipokuwa na wenzake na nani aliyekuwa anawashikilia.

Kwa sasa habari zilizotufikia ni kuwa yupo kituo cha polisi kwa taratibu za kipolisi kwa kuwa jalada la kupotea kwao lilifunguliwa hapo.

Kupatikana kwao kumefuatia wito mkubwa uliokuwa umetolewa na wasanii na mashabiki nchini kuhusu kuachiliwa kwake huru, ndani na nje ya mitandao ya kijamii.

Kabla ya hapo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Simon Sirro alitoa tamko kwamba bado walikuwa wakiendelea na upelelezi wa tukio la kupotea kwa msanii huyo na wenzake.

XS
SM
MD
LG