Siku moja baada ya makombora ya Tomahawk 59 kupigwa katika uwanja wa ndege wa Shayrat, Syria, maafisa wa ngazi ya juu wa Marekani wamesema walikuwa wanatafuta ushahidi ilikujua kwamba utawala wa Syria hakufanya shambulizi hilo peke yake.
“Tunafikiria tunasura kamili juu ya nani aliowasaidia,” afisa wa jeshi wa ngazi ya juu wa Marekani ameiambia Wizara ya Mambo ya Nje, akiongeza kuwa maafisa wao “wanafanya tathmini kwa makini kabisa taarifa yoyote ambayo inaweza kuihusiha Russia”—wakithibitisha kuwa kati ya mambo mawili Russia ilikuwa inajua kuhusu shambulizi hilo la Jumanne au walilisaidia jeshi la serikali ya Syria kufanya hilo.
Maoni ya Wizara hiyo Ijumaa yamekuja baada ya mlolongo wa muhtasari wa ukosoaji kutoka Washington kuhusu jukumu la Russia nchini Syria, baadhi zikiituhumu Moscow kuwa inajaribu “kuwachanganya” juu ya suala la Syria kutumia silaha zakemikali kwa kunadi kile wanachokiita ni “habari za uongo.”'’
'Russia lazima ichague'
“Damascus na Moscow walituhakikishia kuwa silaha hizi zote zilikuwa zimeondolewa na kuteketezwa,” afisa wa Marekani ameiambia VOA, akigusia mkataba wa 2013 wakutokomeza mrundiko wa silaha za kemikali za Syria.
“Russia inakabiliwa na chaguo,” afisa huyo aliongeza. “Ni kati ya kuchukua jukumu kuhakikisha silaha hizo zinaondolewa kama Russia ilivyokuwa imeahidi kufanya hivyo, au ikubali kuwa haina uwezo wa kumdhibiti Rais wa Syria Bashar al-Assad.”
Hata hivyo maafisa wa Pentagon wamekataa kutoa ushahidi wa moja kwa moja Ijumaa unaoonyesha Russia ilihusika na shambulizi hilo la gesi Aprili 4 katika mji wa Khan Sheikhoun, ambao ulishambuliwa na mabomu ya kemikali ya sarin, ambayo ni kemikali yenye nguvu na ni hatarishi kwa mishipa ya fahamu.
Lakini pia wamesema kuwa kituo cha jeshi la anga la Russiakiko katika uwanja wa ndege huo huo, na kuwa vikosi vya Russia huko Syria vinajulikana kuwa na utaalamu wa silaha za kemikali.