Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 00:48

Msako wa silaha waleta wasiwasi Burundi

Wanajeshi na wapolisi katika mji ya Bujumbura, nchini Burundi.
Wanajeshi na wapolisi katika mji ya Bujumbura, nchini Burundi.

Nchini Burundi shughuli za maisha ya kila siku kama vile mashule, maduka na shughuli nyingine za kijamii zimesimama katika mitaa ya Cibitoke na Mtakula kufuatia msako wa silaha unaofanywa na jeshi na polisi nchini humo.

Msako wa silaha Burundi
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:56 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Nchini Burundi shughuli za maisha ya kila siku kama vile mashule, maduka na shughuli nyingine za kijamii zimesimama katika mitaa ya Cibitoke na Mtakula kufuatia msako wa silaha unaofanywa na jeshi na polisi nchini humo.

Idadi kubwa ya wakazi wa kata hizo ambao wengi walishiriki katika maandamano ya kupinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza walihamia katika maeneo mengine ya mji wa Bujumbura kwa kuhofia ghasia ambazo zinaweza kuzuka wakati polisi wanawapokonya watu wenye silaha kwa nguvu.

Wakazi wa eneo hilo wanasema hata maduka ya vifaa vya kawaida vya nyumbani yamefungwa kiasi kwamba wengi katika mitaa hiyo wanashindwa kujikimu kimaisha.

Jumanne ni siku ya tatu tangu serikali itoe muda wa siku tano kwa wenye silaha kuzisalimisha. Mpaka sasa polisi wanasema silaha 20 za aina mbali mbali, maguruneti na vifaa vya mawasiliano ya kijeshi yamekamatwa mpaka sasa.

XS
SM
MD
LG