Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 16:31

Burundi hali si shwari


Mwanamme wa kirundi akiwa amebeba mizigo yake, akikimbia kutoka mji mkuu Bujumbura kwa kukhofia kuzuka tena kwa ghasia.
Mwanamme wa kirundi akiwa amebeba mizigo yake, akikimbia kutoka mji mkuu Bujumbura kwa kukhofia kuzuka tena kwa ghasia.

Watu waliokuwa na silaha walivamia baa moja katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura Jumamosi usiku na kuua takriban watu saba.

Walioshuhudia wamesema washambuliaji waliwaamuru watu ambao walikuwa wamekaa nje kuingia ndani ya jengo; halafu wavamizi hao wakaanza kufyatua risasi. Walioshuhudia wameliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa washambuliaji walikuwa wamevalia sare za polisi.

Wasi wasi wa kimataifa unazidi kuongezeka kwasababu ya kuongezeka kwa ghasia katika taifa hilo la afrika ya Kati kufuatia Rais Pierre Nkurunziza kuchaguliwa tena kuongoza nchi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, John Kirby katika taarifa yake siku ya Jumamosi, amesema Marekani ina wasi wasi mkubwa kwamba "matamshi ya karibuni ya kichochezi" yaliyotolewa na baadhi ya maafisa wa serikali na mpango wa msako wa mwishoni mwa wiki uliotolewa na Nkurunziza "unazidisha hatari ya kuzuka kwa ghasia kubwa nchini Burundi."

Rais wa Marekani, Barack Obama anasema anapanga kuiondoa Burundi kutoka kwenye program ya biashara na Marekani kwasababu ya hali mbaya ya ukamataji unaowakumba wanasiasa wa upinzani nchini humo, baada ya Nkurunziza kurejea tena madarakani.

Uamuzi wa Nkurunzia kuwania awamu ya tatu ya uongozi ulichochea ghadhabu kutoka kwa warundi wengi ambao wamesema alikiuka katiba na mkataba wa Arusha ambao ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya takriban miaka 13.

XS
SM
MD
LG