Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:41

Msajili wa vyama vya siasa Tanzania alaumiwa na CUF


Leader of opposition Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad
Leader of opposition Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad

Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi ameendelea kulalamikiwa na chama cha upinzani CUF nchini Tanzania kutokana na kile wanachodai kuwa ni hujuma anazozifanya dhidi ya chama hicho.

Mutungi amelaumiwa na Katibu Mkuu wa CUF kuwa amekuwa akishirikiana na Profesa Ibrahim Lipumba kukihujumu chama hicho.

Maalim Seif alieleza hayo Ijumaa katika barua yake ya kumjibu Jaji Mutungi kuhusu hatua yake ya kuwatambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti halali wa CUF na Magdalena Sakaya kama kaimu katibu mkuu pamoja na kuwa watu hao tayari walishasimamishwa uanachama kwa tuhuma mbalimbali.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Tanzania Katibu mkuu huyo alifikia uamuzi wa kumjibu Jaji Mutungi baada ya ombi lake la kuwafukuza uanachama wabunge wawili; Sakaya (Kaliua) na Maftaha Nachuma (Mtwara Mjini) kugonga ukuta.

Madai ya CUF ni kuwa Profesa Lipumba alimweleza Msajili kuwa Maalim Seif ameshindwa kutekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kutofika ofisi ya chama hicho zilizopo Buguruni, hivyo akamteua Sakaya ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Bara kukaimu ukatibu mkuu.

“Kwa mujibu wa katiba ya CUF mimi, Maalim Seif bado ni katibu mkuu wa chama hiki na nipo hapa nchini, ni mzima na nina akili timamu. Na nafasi yangu haiwezi kukaimiwa na Sakaya ambaye tulishamsimamisha uanachama,” inaeleza barua hiyo.

​
XS
SM
MD
LG