Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 13:11

Moto mkubwa unaoteketeza misitu washindwa kudhibitiwa California


Gari la zimamoto likiwa katika njia kuu namba 96 huku eneo la McKinney likiendelea kuungua katika Msitu wa Taifa wa Klamath California, July 30, 2022.

Maafisa wanaokabiliana na moto mkubwa  unaoendelea kuteketeza misitu Carlifonia, wanakumbana na hali ngumu  kutokana na radi pamoja na joto la hali ya juu, vinavyoongeza moto kusambaa, huku wakifanya kila juhudi kulinda jamii.

Msemaji wa idara ya kitaifa ya misitu, Aderienne Freeman, amesema kwamba moto mkubwa unaendela kuteketeza sehemu za Mckinney, katika msitu wa kitaifa wa Klamath, North Carolina.

Ukubwa wa moto huo umeongezeka na kuenea hadi umbali wa kilomita 207 mraba, siku mbili baada ya kuripotiwa katika kaunti ya Siskiyou, yenye idadi ndogo ya watu.

Uchunguzi unaendelea kubaini kilichosababisha moto huo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG