Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 04:48

Moscow yadai kuanza kusafirisha nafaka bure kwenda Afrika


Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa Saint Petersburg, Novemba 17, 2023. Picha na Reuters
Rais wa Russia Vladimir Putin akiwa Saint Petersburg, Novemba 17, 2023. Picha na Reuters

Waziri wa kilimo wa Russia amesema kwamba Moscow imeanza kusafirisha nafaka za bure kiasi cha tani 200,000 kwa nchi sita za Afrika kama alivyoahidi rais Vladimir Putin mnamo mwezi Julai.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa Instagram, Dmitry Patrushev, amesema kwamba meli zilizobeba nafaka hizo ziko njiani kuelekea Burkina Faso na Somalia na kwamba nafaka zaidi zitasafirishwa hivi karibuni kuelekea Eritrea, Zimbabwe, Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Putin aliahidi kutoa nafasa ya bure kwa nchi sita wakati wa kikao na viongozi kutoka Afrika mnamo mwezi July, baada ya Moscow kujiondoa kutoka makubaliano ya kusafirisha nafasa, yaliyowezesha Ukraine kusafirisha kutoka bandari zake za bblack swa licha ya kuendelea kwa vita vya Russia nchini humo.

Makubaliano ya kusafirisha nafaka yalikuwa yamesaidia kupunguza bei ya nafaka katika masoko ya kimataifa lakini Putin alidai kwamba yameshindwa kuhakikisha kwamba nafaka zinafika katika nchi ambazo zinahitaji zaidi nafaka hizo.

Russia imeishambulia Ukraine kwa mabomu kila mara na kuharibu ghala za nafaka tangu ilipojiondoa kwenye makubaliano hayo. Ukraine imesema kwamba maelfu ya tani za nafaka zimeharibiwa.

Ukraine hata hivyo imesema Ijumaa kwamba imefanikiwa kusafirisha tani milioni 4.4 za shehena ikiwemo tani milioni 3.2 za nafaka tangu Agosti kupitia njia salama ambayo iliunda.

Forum

XS
SM
MD
LG