Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:10

Moscow yafikiria kuchukua hatua dhidi ya Marekani


Rais Trump na Rais Putin
Rais Trump na Rais Putin

Naibu Waziri wa mMambo ya Nje wa Russia Serge Ryabkov amesema huenda Moscow ikachukua hatua dhidi ya Marekani.

Hatua hiyo ya Russia ni majibu ya vikwazo vipya ambavyo Washington imeiwekea kwa kuiadhibu kutokana na madai ya kuingilia uchaguzi wa urais wa mwaka 2016.

Baraza la Wawakilishi la Marekani Jumanne liliidhinisha sheria ambayo inaoongeza uwezo wa bunge kudhibiti uwezo wa Rais wa Marekani Donald Trump kupunguza hatua za vikwazo zilizochukuliwa dhidi ya Russia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la serikali ya Russia , Ryabkov ameonya kuwa vikwazo hivyo huenda vikavuruga uwezekano wa kuboresha uhusiano kati ya Moscow na Washington.

Ameeleza pia kwamba Russia iliuonya utawala wa Trump kuwa watajibu mapigo endapo wabunge wa Marekani watapitisha mswaada huo.

mswaada huo ulipitishwa kwa kura 419 kwa 3 ikijumuisha vikwazo dhidi ya Iran na Korea Kaskazini pamoja na Russia kuhusiana na masuala mbali mbali.

XS
SM
MD
LG