Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 25, 2020 Local time: 14:11

Mkwe wa Trump anatarajiwa kutoa ushuhuda juu ya Russia


Kushner akiwa na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas

Uchunguzi juu ya Russia kuingilia kati uchaguzi wa Marekani umeingia katika hatua mpya wiki hii wakati kamati za bunge zikiendelea kutafuta taarifa kutoka kwa wanafamilia wawili wa Donald Trump.

Mmoja wao ni mkwe wake Trump, Jared Kushner, ambaye anatarajiwa kuhojiwa katika Bunge la Marekani Jumatatu.

Mtu ambaye anaonekana mara nyingi lakini nadra kusikika, Kushner ni mmoja wa washauri wa karibu wa Rais Donald Trump.

Pia Kushner amepewa dhima ya kufuatilia suala la amani la Mashariki ya Kati na kuongoza juhudi za kubadilisha mifumo ya serikali iwe ya kisasa.

Kushner amepagiwa kukutana Jumatatu katika kikao cha faragha na Kamati ya Usalama ya Baraza la Seneti na Jumanne atahojiwa na Kamati ya Upelelezi ya Bunge.

Majopo yote mawili yanatarajiwa kutaka kujua taarifa kuhusu mawasiliano yake na Russia, ikiwemo mkutano aliofanya na balozi wa Russia nchini Marekani na mwezi Juni uliopita mkutano wake na mwanasheria wa Russia na watu wengine wenye mafungamano na Moscow.

Mkutano huo umekuwa ukiangazwa kwa hamu kubwa kwani mtoto wa Rais, Donald Trump Jr, aliweka wazi barua pepe zinazoelezea kuridhishwa kwakw na kile alichoamini kuwa mwanasheria wa Russia atatoa taarifa zitakazo mhujumu Hillary Clinton, ambaye ni hasimu wa kisiasa wa Trump katika uchaguzi wa mwaka 2016.

Facebook Forum

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG